Leviticus 13:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama kuhani atamwangalia huyo mtu na kuona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na wala hakuna shimo, ila pamefifia, basi, atamtenga huyo mtu kwa muda wa siku saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa kuhani anapopachunguza pakawa hapana nywele nyeupe ndani yake, wala hapakuingia ndani ya ngozi, na pameanza kupungua, basi kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kuhani akipaangalia, na tazama hamna malaika meupe ndani yake, wala hapana pa kuingia ndani kuliko ile ngozi, lakini paanza kufifia, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama kuhani atamwangalia huyo mtu na kuona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na wala hakuna shimo, ila pamefifia, basi, atamtenga huyo mtu kwa muda wa siku saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa wakati kuhani anapopachunguza pakawa hapana nywele nyeupe ndani yake wala hakuna shimo, bali pamepungua, basi kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa wakati kuhani anapopachunguza pakawa hapana nywele nyeupe ndani yake, wala hakuna shimo bali pamepungua, basi kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhani akipaangalia, na iwe hamna nywele nyeupe ndani yake, wala hapakuingia ndani kuliko ile ngozi, lakini panaanza kufifia, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama kuhani atamwangalia huyo mtu na kuona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na wala hakuna shimo, ila pamefifia, basi, atamtenga huyo mtu kwa muda wa siku saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtambikaji akimtazama na kuona, ya kama nywele hazikugeuka kuwa nyeupe, tena hapakubonyea katika ngozi, ila panaanza kufifia, mtambikaji na amfungie siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kuhani akipaangalia, na tazama hamna malaika meupe ndani yake, wala hapana pa kuingia ndani kuliko ile ngozi, lakini paanza kufifia, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama kuhani akimwangalia yule mutu na kuona kwamba nywele za pahali pale si nyeupe na wala hakuna shimo, lakini pamefifia, basi, atamutenga huyu mutu kwa muda wa siku saba.