Leviticus 13:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama kuhani akiona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na hakuna shimo ila pamefifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa muda wa siku saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kuhani akipachunguza na akaona kwamba hakuna nywele nyeupe kwenye alama ile, wala hapakuingia ndani ya ngozi, na pamepungua, basi kuhani atamtenga kwa siku saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kuhani akipaangalia, na tazama, malaika meupe hamna katika hicho kipaku king'aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama kuhani akiona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na hakuna shimo ila pamefifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa muda wa siku saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama kuhani akichunguza na kuona kwamba hakuna nywele nyeupe kwenye alama ile wala hakuna shimo napo pameanza kupungua, basi kuhani atamtenga kwa siku saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama kuhani akichunguza na kuona kwamba hakuna nywele nyeupe kwenye alama ile, wala hakuna shimo napo pameanza kupungua, basi kuhani atamtenga kwa siku saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhani akipaangalia, nywele nyeupe hamna katika hicho kipaku king'aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama kuhani akiona kuwa nywele za mahali hapo si nyeupe na hakuna shimo ila pamefifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa muda wa siku saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtambikaji akipatazama na kuona, ya kama hapo penye balanga hapana nywele nyeupe, wala hapakubonyea katika ngozi, napo panaanza kufifia, mtambikaji na amfungie siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kuhani akipaangalia, na tazama, malaika meupe hamna katika hicho kipaku king’aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama kuhani akiona kwamba nywele za pahali pale si nyeupe na hakuna shimo lakini pamefifia, basi, kuhani atamutenga mutu yule kwa muda wa siku saba.