Leviticus 13:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, kama ile alama haijaenea, ila imefifia, huo ni uvimbe uliotokana na kuungua; basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi; kwani hilo ni kovu la kuungua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi, napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto, na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama hicho kipaku kikishangaa pale pale, wala hakikuenea katika ngozi, lakini kimefifia; ni kufura kwake pale penye moto, na kuhani atasema kwamba yu safi; kwa kuwa ni kovu la kuwasha hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, kama ile alama haijaenea, ila imefifia, huo ni uvimbe uliotokana na kuungua; basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi; kwani hilo ni kovu la kuungua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi, napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto, na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama hicho kipaku kikibaki pale pale, wala hakikuenea katika ngozi, lakini kimefifia; ni kufura kwake pale penye moto, na kuhani atasema kuwa ni safi; kwa kuwa ni kovu la kuwasha hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, kama ile alama haijaenea, ila imefifia, huo ni uvimbe uliotokana na kuungua; basi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi; kwani hilo ni kovu la kuungua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama hilo balanga ni lilelile mahali pake, halikuendelea katika ngozi, ila limeanza kufifia basi, ndio kivimbe cha kidonda cha moto tu, naye mtambikaji hana budi kusema, ya kama ametakata, kwani ni kovu tu la kidonda cha moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama hicho kipaku kikishangaa pale pale, wala hakikuenea katika ngozi, lakini kimefifia; ni kufura kwake pale penye moto, na kuhani atasema kwamba yu safi; kwa kuwa ni kovu la kuwasha hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, kama ile alama haijaenea, lakini imefifia, hicho ni kivimba kilichotokana na kuungua. Basi, kuhani atamutangaza mutu yule kuwa safi, maana hilo ni kovu la kuungua.