Leviticus 13:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atapakagua mahali palipo na ugonjwa na ikiwa nywele za mahali hapo zimebadilika kuwa nyeupe na ugonjwa wenyewe ukionekana kuwa uko ndani zaidi ya ngozi ya mwili wake, basi, huo ni ukoma. Kuhani akimaliza kumkagua, hivyo atatangaza kuwa mtu huyo ni najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake, na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe, na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na kwamba malaika yaliyo katika hilo pigo yamegeuka kuwa meupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na kuhani atamwangalia na kusema kuwa yu mwenye unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atapakagua mahali palipo na ugonjwa na ikiwa nywele za mahali hapo zimebadilika kuwa nyeupe na ugonjwa wenyewe ukionekana kuwa uko ndani zaidi ya ngozi ya mwili wake, basi, huo ni ukoma. Kuhani akimaliza kumkagua, hivyo atatangaza kuwa mtu huyo ni najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa ni najisi kwa kawaida ya ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake, na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe, na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa ni najisi kwa kawaida ya ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na nywele zilizoko katika hilo pigo zimegeuka kuwa nyeupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na ikiwa nywele zilizoko katika sehemu zilizougua zimegeuka rangi na kuwa nyeupe, na hilo pigo kuonekana limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili, hilo ni pigo la ukoma,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atapakagua mahali palipo na ugonjwa na ikiwa nywele za mahali hapo zimebadilika kuwa nyeupe na ugonjwa wenyewe ukionekana kuwa uko ndani zaidi ya ngozi ya mwili wake, basi, huo ni ukoma. Kuhani akimaliza kumkagua, hivyo atatangaza kuwa mtu huyo ni najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji akilitazama hilo doa la ngozi ya mwili, akiona, ya kuwa nywele penye hilo doa zimegeuka kuwa nyeupe, tena hilo doa likionekana kuwa linabonyea katika ngozi nyingine ya mwili, basi, ndio doa la ukoma; mtambikaji akiisha kumwona kuwa hivyo hana budi kusema, ya kama ni mwenye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na huyo kuhani ataliangalia hilo pigo lililo katika ngozi ya mwili; na kwamba malaika yaliyo katika hilo pigo yamegeuka kuwa meupe, na hilo pigo kuonekana kwake limeingia ndani kuliko ile ngozi ya mwili wake, ni pigo la ukoma hilo; na kuhani atamwangalia na kusema kuwa yu mwenye unajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atachunguza pahali panapokuwa ugonjwa na ikiwa nywele za pahali pale zimebadilika kuwa nyeupe na ugonjwa wenyewe ukionekana kuwa uko ndani zaidi ya ngozi ya mwili wake, basi, huo ni ukoma. Kuhani akimaliza kumuchunguza, hivyo atatangaza kwamba mutu yule ni muchafu.