Leviticus 13:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani ya ngozi, na nywele zilizo juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; na tazama, kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, tena zikiwamo nywele za rangi ya manjano kisha nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba yu najisi, maana, ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa, au wa ndevu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kuhani atakichunguza kile kidonda na kama ataona kuwa kimeingia ndani na nywele zilizoko juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi, kwani ni upele; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani, na nywele zilizoko juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi, kwani ni upele; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; ikiwa pigo limeingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na nywele zilizomo kuwa za rangi ya manjano na nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi, maana ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa au wa kindevu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kuhani atauangalia ugonjwa huo. Iwapo kuhani ataona kuwa kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mtambikaji akiutazama huo upele na kuona, ya kama unaonekana kuwa unabonyea katika ngozi, ya kama nazo nywele za hapo ni nyekundu kidogo, tena ni nyembamba, mtambikaji hana budi kusema, ya kama ni mwenye uchafu, kwani ndio upele mbaya, maana ukoma wa kichwani na wa kidevuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; na tazama, kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe, tena zikiwamo nywele za rangi ya manjano kisha nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba yu najisi, maana, ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa, au wa ndevu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kuhani ataangalia ugonjwa huo. Ikiwa kuhani ataona kwamba kuna shimo na nywele ni manjano na nyembamba, basi, atamutangaza mutu yule kuwa muchafu, maana huo ni upele na ni ukoma wa kichwa au wa kidevu.