Leviticus 13:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya saba, kuhani ataviangalia vile vipele. Iwapo kuhani ataona kuwa vipele hivyo havikuenea kwenye ngozi na wala havikwenda ndani ya ngozi, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Mtu huyo atafua mavazi yake, naye atakuwa safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba kuhani atachunguza tena kidonda kile; ikiwa hakijaenea kwenye ngozi na hakikuingia ndani ya ngozi, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake, naye atakuwa safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na siku ya saba kuhani atakiangalia hicho kipwepwe, na tazama, ikiwa kipwepwe hakikuenea katika ngozi yake, wala hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi; ndipo huyo kuhani atasema kwamba yu safi; naye atazifua nguo zake, naye atakuwa yu safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya saba, kuhani ataviangalia vile vipele. Iwapo kuhani ataona kuwa vipele hivyo havikuenea kwenye ngozi na wala havikwenda ndani ya ngozi, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Mtu huyo atafua mavazi yake, naye atakuwa safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba kuhani atachunguza tena ule upele; ikiwa kwamba haujaenea kwenye ngozi na hakuna shimo mahali pale, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake naye atakuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba kuhani atachunguza tena ule upele; ikiwa haujaenea kwenye ngozi na hakuna shimo mahali pale, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake, naye atakuwa safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na siku ya saba kuhani atakiangalia hicho kipwepwe, ikiwa kipwepwe hakikuenea katika ngozi yake, wala hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi; ndipo huyo kuhani atasema kwamba ni safi; naye atazifua nguo zake, naye atakuwa ni safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya saba, kuhani ataviangalia vile vipele. Iwapo kuhani ataona kuwa vipele hivyo havikuenea kwenye ngozi na wala havikwenda ndani ya ngozi, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Mtu huyo atafua mavazi yake, naye atakuwa safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji atakapomtazama tena huyu mwenye upele mbaya siku ya saba na kuona, ya kama huo upele mbaya haukuendelea katika ngozi, wala hauonekani kuwa unabonyea katika ngozi, mtambikaji hana budi kusema, ya kama ametakata, naye na azifue nguo zake, kisha atakuwa ametakata kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na siku ya saba kuhani atakiangalia hicho kipwepwe, na tazama, ikiwa kipwepwe hakikuenea katika ngozi yake, wala hakionekani kuingia ndani kuliko ngozi; ndipo huyo kuhani atasema kwamba yu safi; naye atazifua nguo zake, naye atakuwa yu safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya saba, kuhani ataangalia vile vipele. Ikiwa kuhani ataona kwamba vipele hivyo havikuenea kwenye ngozi na wala havikuingia ndani ya ngozi, basi, atamutangaza mutu yule kuwa safi. Mutu huyo atafua nguo zake, naye atakuwa safi.