Leviticus 13:37 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, huyo mtu amepona. Yeye si najisi; kuhani atamtangaza kuwa safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimeshangaa, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini, hata hivyo, katika hukumu yake akiona hapajabadilika na nywele nyeusi zimeota juu yake, upele umepona. Yeye si najisi na kuhani atamtangaza kuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, upele umepona. Yeye si najisi, kuhani atamtangaza kuwa safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimepungua, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akiona kwa macho yake, ya kuwa upele mbaya ni uleule, ya kuwa nywele nyeusi zimeota hapo, basi, upele mbaya umepona, naye mwenyewe ametakata, naye mtambikaji hana budi kusema ya kama ametakata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimeshangaa, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiwa kuhani ataona kwamba vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota pahali pale, basi, vidonda vimepona, basi, mutu yule ni safi. Kuhani atamutangaza mutu yule kuwa safi.