Leviticus 13:42 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upara, au kwenye paji la uso, ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upaa, au kile kipaji kilicho na upaa, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upaa, au katika kipaji chake cha upaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upaa au kwenye paji la uso ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upaa, au kwenye paji la uso, ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upara, au kile kipaji kilicho na upara, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upara, au katika kipaji chake cha upara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini penye kipara cha kisogoni au cha utosini pakitokea vipele vyeupe vyenye damudamu, ndio ukoma unaotoka penye kipara chake cha kisogoni au cha utosini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upaa, au kile kipaji kilicho na upaa, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upaa, au katika kipaji chake cha upaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama kwenye kichwa penye upaa au kwenye paji la uso kwenye upaa kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upaa wake juu ya kichwa au kwenye paji lake.