Leviticus 13:49 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
iwapo upele huo una rangi ya kijani au nyekundu katika vazi hilo, basi, vazi hilo lina upele. Kwa hiyo ni lazima kumwonesha kuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ikiwa maambukizo kwenye vazi, ngozi, au vazi lililofumwa au kusokotwa la kitani au sufu, au kitu chochote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni ukoma unaoenea, na ni lazima kuhani aoneshwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hilo pigo likiwa la rangi ya majani au jekundu, katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi; ni pigo la ukoma, nalo ataonyeshwa kuhani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
iwapo upele huo una rangi ya kijani au nyekundu katika vazi hilo, basi, vazi hilo lina upele. Kwa hiyo ni lazima kumwonesha kuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
tena kama maambukizo kwenye vazi, au ngozi, au lililofumwa au kusokotwa, au kifaa cho chote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni upele unaoenea na ni lazima kuhani aonyeshwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
tena kama maambukizo kwenye vazi, au ngozi, au lililofumwa au kusokotwa, au kifaa chochote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni upele unaoenea na ni lazima kuhani aonyeshwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hilo pigo likiwa la rangi ya kijani au jekundu, katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi; ni pigo la ukoma, nalo ataoneshwa kuhani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
iwapo upele huo una rangi ya kijani au nyekundu katika vazi hilo, basi, vazi hilo lina upele. Kwa hiyo ni lazima kumwonesha kuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
zote pia hupatwa na ukoma: madoadoa ya kimajanijani au ya damudamu yakitoka katika nguo au katika ngozi au katika nyuzi za kufumwa au katika nyuzi za kusokotwa au katika chombo cho chote kilichotengenezwa kwa ngozi, ndio huo ugonjwa mbaya wa ukoma; kwa hiyo sharti utazamwe na mtambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hilo pigo likiwa la rangi ya majani au jekundu, katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi; ni pigo la ukoma, nalo ataonyeshwa kuhani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ikiwa taka lile lina rangi ya kijani au nyekundu katika nguo ile, basi, nguo ile ina ukoma. Kwa hiyo ni lazima kumwonyesha kuhani.