Leviticus 13:51 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya saba atauangalia upele huo. Ikiwa upele huo umeenea katika vazi hilo, liwe ni la kufuma au kusokotwa au la ngozi au la ngozi ya aina yoyote ile, vazi hilo lina upele. Hivyo vazi hilo ni najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba atalichunguza, na kama ukoma umeenea kwenye vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyovyote vile itumikavyo, ni ukoma wa kuangamiza; vazi hilo ni najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha siku ya saba ataliangalia hilo pigo; kama pigo limeenea katika hilo lililofumwa, au katika hilo lililosokotwa, au katika ngozi, ijapokuwa hiyo ngozi ina matumizi yo yote; hilo pigo ni ukoma unaokula; vazi hilo ni najisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya saba atauangalia upele huo. Ikiwa upele huo umeenea katika vazi hilo, liwe ni la kufuma au kusokotwa au la ngozi au la ngozi ya aina yoyote ile, vazi hilo lina upele. Hivyo vazi hilo ni najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba atakichunguza, na kama upele umeenea kwenye nguo, au kifaa kilichofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyo vyote vile itumikavyo, ni upele uangamizao, kifaa hicho ni najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba atakichunguza, na kama upele umeenea kwenye nguo, au kifaa kilichofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyovyote vile itumikavyo, ni upele uangamizao, kifaa hicho ni najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha siku ya saba ataliangalia hilo pigo; kama pigo limeenea katika hilo lililofumwa, au katika hilo lililosokotwa, au katika ngozi, ijapokuwa hiyo ngozi ina matumizi yoyote; hilo pigo ni ukoma unaona; vazi hilo ni najisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya saba atauangalia upele huo. Ikiwa upele huo umeenea katika vazi hilo, liwe ni la kufuma au kusokotwa au la ngozi au la ngozi ya aina yoyote ile, vazi hilo lina upele. Hivyo vazi hilo ni najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Atakapokitazama siku ya saba hicho kilichopatwa na huu ugonjwa mbaya na kuona, ya kama ugonjwa huu mbaya umeendelea katika nguo au katika nyuzi za kufumwa au katika nyuzi za kusokotwa au katika ngozi, ijapo hiyo ngozi iwe imetengenezewa kazi yo yote, basi, ugonjwa huu mbaya ndio ukoma unaokula, nacho kile kitu ni chenye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha siku ya saba ataliangalia hilo pigo; kama pigo limeenea katika hilo lililofumwa, au katika hilo lililosokotwa, au katika ngozi, ijapokuwa hiyo ngozi ina matumizi yo yote; hilo pigo ni ukoma unaokula; vazi hilo ni najisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya saba ataangalia taka lile. Ikiwa taka lile limeenea katika nguo hiyo, ikuwe ni ya kufuma au kusokotwa au ya ngozi au ya ngozi ya aina yoyote, nguo ile ina ukoma. Hivyo nguo ile ni chafu.