Leviticus 13:52 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atalichoma moto vazi hilo kwani lina namna ya upele wa ukoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni lazima achome vazi hilo, liwe ni la sufu au kitani kilichofumwa au kusokotwa, au kitu chochote cha ngozi chenye maambukizo; kwa kuwa ni ukoma wa kuangamiza, vazi lote ni lazima lichomwe moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atalichoma moto vazi hilo, kwamba ni lililofumwa au kwamba ni lililosokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu cho chote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaokula; vazi hilo litachomwa moto;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atalichoma moto vazi hilo kwani lina namna ya upele wa ukoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni lazima aichome hiyo nguo, ikiwa ni ya sufu ama kitani iliyofumwa ama kusokotwa, ama chombo cho chote cha ngozi chenye maambukizo, kwa kuwa ni upele unaoangamiza; chombo chote ni lazima kichomwe moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni lazima aichome hiyo nguo, ikiwa ni ya sufu ama kitani iliyofumwa ama kusokotwa, ama chombo chochote cha ngozi chenye maambukizo, kwa kuwa ni upele unaoangamiza; chombo chote ni lazima kichomwe moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ataliteketeza vazi hilo, liwe ni la kufumwa au ni la kusokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu chochote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaona; vazi hilo litateketezwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atalichoma moto vazi hilo kwani lina namna ya upele wa ukoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti waziteketeze hizo nguo au hizo nyuzi za kufumwa au hizo nyuzi za kusokotwa, kama ni za nywele za kondoo au za pamba, navyo vyo vyote vilivyotengenezwa kwa ngozi vilivyo vyenye ugonjwa huo mbaya, kwani ndio ukoma unaokula; kwa hiyo sharti viteketezwe kwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atalichoma moto vazi hilo, kwamba ni lililofumwa au kwamba ni lililosokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu cho chote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaokula; vazi hilo litachomwa moto;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atachoma kwa moto nguo ile maana ina namna ya ukoma wenye kuenea.