Leviticus 13:55 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani ataliangalia hilo vazi baada ya kuoshwa. Ikiwa ile alama haijabadilika rangi yake hata ingawa upele haukuenea, basi, vazi hilo ni najisi. Vazi hilo utalichoma moto, iwe alama ya upele ipo nyuma au mbele ya vazi hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya vazi lenye maambukizo kusafishwa, kuhani atalichunguza, na kama ukoma haujaonesha badiliko lolote, hata kama haujaenea, ni najisi. Lichome kwa moto, iwe ukoma umeenea upande mmoja au mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; na tazama, ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, li najisi; utakichoma moto; ni uharibifu likiwa lina upaa ndani au nje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani ataliangalia hilo vazi baada ya kuoshwa. Ikiwa ile alama haijabadilika rangi yake hata ingawa upele haukuenea, basi, vazi hilo ni najisi. Vazi hilo utalichoma moto, iwe alama ya upele ipo nyuma au mbele ya vazi hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kifaa chenye maambukizo kusafishwa, kuhani atakichunguza, na kama upele hujaonyesha badiliko lo lote, hata kama haujaenea, ni najisi. Choma kwa moto, kama upele umeenea upande mmoja au mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kifaa chenye maambukizo kusafishwa, kuhani atakichunguza, na kama upele haujaonyesha badiliko lolote, hata kama haujaenea, ni najisi. Kichome kwa moto, iwe upele umeenea upande mmoja au mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, ni najisi; utaliteketeza; ni uharibifu likiwa lina doa ndani au nje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani ataliangalia hilo vazi baada ya kuoshwa. Ikiwa ile alama haijabadilika rangi yake hata ingawa upele haukuenea, basi, vazi hilo ni najisi. Vazi hilo utalichoma moto, iwe alama ya upele ipo nyuma au mbele ya vazi hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtambikaji atakapovitazama vilivyopatwa na ugonjwa huo mbaya, vikiisha kufuliwa, na kuona, ya kama hapo penye ugonjwa huo mbaya hapakugeuka kuwa namna nyingine, ijapo ugonjwa wenyewe uwe haukuendelea, basi, ni vichafu, sharti waviteketeze kwa moto, kwani mahali hapo panabonyea upande wa nyuma na wa mbele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; na tazama, ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, li najisi; utakichoma moto; ni uharibifu likiwa lina upaa ndani au nje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani ataangalia nguo ile kisha kufuliwa. Ikiwa ile alama haijabadilika rangi yake hata ingawa taka halikuenea, basi, nguo ile ni chafu. Nguo ile utaichoma kwa moto, ikuwe alama ile iko nyuma au mbele ya nguo ile.