Leviticus 13:57 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, ikiwa hiyo alama inaonekana tena baadaye katika vazi lililofumwa au lililosokotwa au katika kitu chochote cha ngozi, basi upele umeenea. Hapo vazi hilo utalichoma moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikijitokeza tena kwenye vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, ama kitu cha ngozi, ule ni ukoma unaoenea; chochote chenye ukoma ni lazima kichomwe kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha, likionekana li vivyo katika hilo vazi, katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi, ni pigo lenye kuenea; nawe vazi hilo lenye pigo utalichoma moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, ikiwa hiyo alama inaonekana tena baadaye katika vazi lililofumwa au lililosokotwa au katika kitu chochote cha ngozi, basi upele umeenea. Hapo vazi hilo utalichoma moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama ikijitokeza tena kwenye nguo au kitu kilichofumwa au kusokotwa, ama kifaa cha ngozi, kwamba ule upele unaenea, cho chote chenye upele ni lazima kichomwe kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama ikijitokeza tena kwenye nguo au kitu kilichofumwa au kusokotwa, ama kifaa cha ngozi, kwamba ule upele unaenea, chochote chenye upele ni lazima kichomwe kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha, likionekana liko vile vile katika hilo vazi, katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, ni pigo lenye kuenea; nawe vazi hilo lenye pigo utaliteketeza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, ikiwa hiyo alama inaonekana tena baadaye katika vazi lililofumwa au lililosokotwa au katika kitu chochote cha ngozi, basi upele umeenea. Hapo vazi hilo utalichoma moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ugonjwa huo ukionekana tena katika hizo nguo au katika hizo nyuzi za kufumwa au katika hizo nyuzi za kusokotwa au katika hivyo vyombo vyo vyote vya ngozi, kama unatokea humo tena, na wavichome moto vilivyopatwa na ugonjwa huo mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha, likionekana li vivyo katika hilo vazi, katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi, ni pigo lenye kuenea; nawe vazi hilo lenye pigo utalichoma moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, ikiwa hiyo alama inaonekana tena kisha katika nguo iliyofumwa au iliyosokotwa au katika kitu chochote cha ngozi, basi ukoma umeenea. Kwa hiyo nguo ile utaichoma kwa moto.