Leviticus 13:59 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiyo ni sheria kuhusu namna ya upele wa ukoma unaotokea katika vazi la sufu au kitani au lililofumwa au lililosokotwa au la ngozi. Kwa njia hiyo mtaweza kupambanua kati ya vazi lisilo najisi na lile lililo najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio masharti kuhusu maambukizo ya ukoma kwenye mavazi ya sufu au kitani, mavazi yaliyofumwa au kusokotwa, ama kitu chochote cha ngozi, kwa ajili ya kuvitangaza kuwa safi au najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiyo ni sheria kuhusu namna ya upele wa ukoma unaotokea katika vazi la sufu au kitani au lililofumwa au lililosokotwa au la ngozi. Kwa njia hiyo mtaweza kupambanua kati ya vazi lisilo najisi na lile lililo najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ni masharti kuhusu maambukizo ya upele kwenye mavazi ya sufu au kitani, yaliyofumwa ama kusokotwa, ama kifaa cho chote cha ngozi, kwa ajili ya kuvitangaza kuwa safi au najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ni masharti kuhusu maambukizo ya upele kwenye mavazi ya sufu au kitani, yaliyofumwa ama kusokotwa, ama kifaa chochote cha ngozi, kwa ajili ya kuvitangaza kuwa safi au najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiyo ni sheria kuhusu namna ya upele wa ukoma unaotokea katika vazi la sufu au kitani au lililofumwa au lililosokotwa au la ngozi. Kwa njia hiyo mtaweza kupambanua kati ya vazi lisilo najisi na lile lililo najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya ugonjwa mbaya wa ukoma, ukishika nguo, kama ni za nywele za kondoo au za pamba, au nyuzi za kufumwa au nyuzi za kusokotwa au vyombo vyo vyote vya ngozi, wapate kusema, ya kama ni vyenye kutakata au vyenye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu cho chote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo ni sheria juu ya taka la ukoma linalotokea katika nguo ya sufu au kitani au iliyofumwa au iliyosokotwa au ya ngozi. Kwa njia hiyo mutaweza kutia tofauti kati ya nguo isiyokuwa chafu na ile inayokuwa chafu.