Leviticus 14:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku ya nane ataleta wanakondoo madume wawili wasio na dosari, kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na dosari, kilo tatu za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka pamoja na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja ya mafuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili waume wakamilifu, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza mkamilifu, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku ya nane ataleta wanakondoo madume wawili wasio na dosari, kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na dosari, kilo tatu za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka pamoja na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja ya mafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja ya mafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo dume wawili wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja jike wa mwaka wa mmoja asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku ya nane ataleta wanakondoo madume wawili wasio na dosari, kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na dosari, kilo tatu za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka pamoja na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya nane na achukue wana kondoo wawili wasio na kilema na kondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na kilema na vibaba kumi vya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko na nusu kibaba ya mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili waume wakamilifu, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza mkamilifu, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya nane ataleta wana-kondoo dume wawili wasiokuwa na kilema, kondoo dike wa mwaka mumoja asiyekuwa na kilema, kilo tatu za unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya vyakula pamoja na mafuta sehemu moja ya tatu ya litre.