Leviticus 14:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha atamchinja huyo mwanakondoo katika mahali patakatifu, wanapochinjia wanyama wa sadaka ya kuondoa dhambi na sadaka ya kuteketezwa. Sadaka hii ya kuondoa hatia, kama ilivyo sadaka ya kuondoa dhambi, ni mali yake kuhani; ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjiwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; ni takatifu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ni vivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha atamchinja huyo mwanakondoo katika mahali patakatifu, wanapochinjia wanyama wa sadaka ya kuondoa dhambi na sadaka ya kuteketezwa. Sadaka hii ya kuondoa hatia, kama ilivyo sadaka ya kuondoa dhambi, ni mali yake kuhani; ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; nayo ni takatifu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjiwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; nayo ni takatifu sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjiapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ndivyo ilivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha atamchinja huyo mwanakondoo katika mahali patakatifu, wanapochinjia wanyama wa sadaka ya kuondoa dhambi na sadaka ya kuteketezwa. Sadaka hii ya kuondoa hatia, kama ilivyo sadaka ya kuondoa dhambi, ni mali yake kuhani; ni sadaka takatifu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha na amchinje huyu mwana kondoo hapo mahali patakatifu, wanapochinja ng'ombe za tambiko za weuo nazo za kuteketezwa nzima. Kwani ng'ombe ya tambiko ya upozi ni yake mtambikaji kama ile ya weuo, ni takatifu yenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ni vivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.