Leviticus 14:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atachovya kidole cha mkono wake wa kulia katika mafuta hayo na kumnyunyizia huyo mtu anayetakaswa mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na achovye kidole chake cha shahada cha mkono wake wa kuume kwenye mafuta yaliyo kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho anyunyize mafuta hayo mara saba mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kuume katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za Bwana;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atachovya kidole cha mkono wake wa kulia katika mafuta hayo na kumnyunyizia huyo mtu anayetakaswa mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
atachovya kidole chake cha mkono wa kuume kwenye mafuta yaliyoko kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho atamnyunyizia mtu yule anayetakaswa mara saba mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na achovye kidole chake cha shahada cha mkono wake wa kuume kwenye mafuta yaliyoko kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho anyunyize mafuta hayo mara saba mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kulia katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atachovya kidole cha mkono wake wa kulia katika mafuta hayo na kumnyunyizia huyo mtu anayetakaswa mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mtambikaji na akichovye kidole chake cha kuume katika mafuta yaliyomo katika gao lake la kushoto, ayanyunyize mara saba mafuta hayo kwa kidole chake mbele ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kuume katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atachovya kidole cha mukono wake wa kuume katika mafuta hayo na kumunyunyizia yule mutu anayetakaswa mara saba mbele ya Yawe.