Leviticus 14:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kiasi cha mafuta yanayobaki katika kiganja chake atampaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia na kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atampaka yule anayetakaswa sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio lake la kuume, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kuume, juu ya damu ya sadaka ya hatia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kiasi cha mafuta yanayobaki katika kiganja chake atampaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia na kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atampaka sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume, mahali pale pale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atampaka yule anayetakaswa sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio lake la kuume, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole gumba cha mguu wake wa kulia, juu ya damu ya sadaka ya hatia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kiasi cha mafuta yanayobaki katika kiganja chake atampaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia na kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo mafuta yatakayosalia gaoni mwake mtambikaji mengine na ayatumie kumpaka mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume na dole gumba la mkono wake wa kuume nalo dole gumba la mguu wake wa kuume juu ya damu ya ng'ombe ya tambiko ya upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kuume, juu ya damu ya sadaka ya hatia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu ya mafuta yanayobaki katika kigaja chake ataipakaa mutu yule anayetakaswa katika incha ya sikio lake la kuume na kidole gumba cha mukono wake wa kuume na kidole gumba cha muguu wake wa kuume, pahali palepale alipomupakaa damu ya sadaka kwa ajili ya kosa.