Leviticus 14:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini, hana uwezo wa kutoa vitu hivyo, basi ataleta mwanakondoo dume mmoja kuwa fidia ya sadaka ya kuondoa hatia ambaye atafanyiwa ishara ya kutoa sadaka ili kumfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho. Ataleta pia kilo moja ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, lazima achukue mwana-kondoo wa kiume mmoja kuwa sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho, pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka, logi moja ya mafuta,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwamba ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini, hana uwezo wa kutoa vitu hivyo, basi ataleta mwanakondoo dume mmoja kuwa fidia ya sadaka ya kuondoa hatia ambaye atafanyiwa ishara ya kutoa sadaka ili kumfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho. Ataleta pia kilo moja ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, ni lazima achukue mwana-kondoo mmoja kama sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na logi moja ya mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, lazima achukue mwana-kondoo mmoja kama sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho, pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na logi moja ya mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo dume mmoja, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini ikiwa mtu huyo ni maskini, hana uwezo wa kutoa vitu hivyo, basi ataleta mwanakondoo dume mmoja kuwa fidia ya sadaka ya kuondoa hatia ambaye atafanyiwa ishara ya kutoa sadaka ili kumfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho. Ataleta pia kilo moja ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka na mafuta theluthi moja ya lita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akiwa mkiwa, mkono wake usiyafikilie haya, basi, na achukue mwana kondoo mmoja tu kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kupitishwa motoni, ajipatie upozi, na vibaba vitatu tu vya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko na nusu kibaba ya mafuta,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwamba ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiwa mutu yule ni masikini, hana uwezo wa kutoa vitu hivyo, basi ataleta mwana-kondoo dume mumoja kuwa malipo ya sadaka kwa ajili ya kosa ambaye atafanyiwa kitambulisho cha kutoa sadaka kwa kumufanyia yule mutu ibada ya upatanisho. Ataleta vilevile kilo moja ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya vyakula na mafuta sehemu moja ya tatu ya litre.