Leviticus 14:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Kisha ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kuume;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia pia ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule atakayetakaswa, ataipaka pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wa kuume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Pia ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole gumba cha mguu wake wa kulia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha na amchinje huyu mwana kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya upozi, kisha mtambikaji na achukue damu kidogo ya hiyo ng'ombe ya tambiko ya upozi, ampake mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume na dole gumba la mkono wake wa kuume nalo dole gumba la mguu wake wa kuume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la huyo atakayetakaswa, na katika chanda cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kuume;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atachinja yule mwana-kondoo dume wa sadaka kwa ajili ya kosa. Kuhani atatwaa sehemu ya damu na kumupakaa yule mutu anayetakaswa katika incha ya sikio lake la kuume, katika kidole gumba cha mukono wake wa kuume na kidole gumba cha muguu wake wa kuume.