Leviticus 14:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hua atakuwa kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Pamoja na hao, atatoa sadaka ya nafaka; naye kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya yule anayetakaswa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hua atakuwa kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Pamoja na hao, atatoa sadaka ya nafaka; naye kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya yule anayetakaswa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele za bwana kwa ajili ya yule anayetakaswa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hua atakuwa kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Pamoja na hao, atatoa sadaka ya nafaka; naye kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa, mkono wake yule ulioweza kuwatoa, mmoja awe ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko; hivyo ndivyo, mtambikaji atakavyompatia mwenye kueuliwa upozi mbele ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hua atakuwa kwa ajili ya sadaka ya zambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Pamoja na hao, atatoa sadaka ya vyakula. Kuhani atamufanyia mutu yule ibada ya upatanisho mbele ya Yawe.