Leviticus 14:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani ataamuru vitu vyote ndani ya nyumba hiyo vitolewe kabla yeye mwenyewe hajaanza uchunguzi wake; visije vyote kutangazwa kuwa najisi. Kisha kuhani ataingia kuiangalia nyumba hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba, kabla hajaenda kuchunguza kama ina ukoma huo, ili kitu chochote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili, kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, mbele ya kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili kwamba vyote vilivyomo nyumbani visiwekwe kuwa unajisi; kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aitazame;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani ataamuru vitu vyote ndani ya nyumba hiyo vitolewe kabla yeye mwenyewe hajaanza uchunguzi wake; visije vyote kutangazwa kuwa najisi. Kisha kuhani ataingia kuiangalia nyumba hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba kabla hajaenda kuchunguza kama ina ugonjwa huo, ili kitu cho chote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba, kabla hajaenda kuchunguza kama ina ugonjwa huo, ili kitu chochote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili, kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, kabla kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili vyote vilivyomo nyumbani visiwe najisi, kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aikague;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani ataamuru vitu vyote ndani ya nyumba hiyo vitolewe kabla yeye mwenyewe hajaanza uchunguzi wake; visije vyote kutangazwa kuwa najisi. Kisha kuhani ataingia kuiangalia nyumba hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji na aagize, watoe humo nyumbani yaliyomo, yeye mtambikaji akiwa hajafika bado kuutazama huo ugonjwa mbaya, kusudi yote yaliyomo humo nyumbani yasipate kuwa yenye uchafu. Baadaye mtambikaji na aingie kuitazama hiyo nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, mbele ya kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili kwamba vyote vilivyomo nyumbani visiwekwe kuwa unajisi; kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aitazame;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani ataamuru vitu vyote ndani ya nyumba hiyo viondoshwe mbele yeye mwenyewe hajaanza uchunguzi wa taka lile, visipate vyote kutangazwa kuwa vichafu. Kisha kuhani ataingia kwa kuiangalia nyumba hiyo.