Leviticus 14:45 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyumba hiyo ni lazima ibomolewe na mawe yake, miti yake na lipu vipelekwe mahali najisi nje ya mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na chokaa yote; vyote vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hata mahali palipo na uchafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyumba hiyo ni lazima ibomolewe na mawe yake, miti yake na lipu vipelekwe mahali najisi nje ya mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na lipu yake, vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na lipu yake, vyote vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hadi mahali palipo na uchafu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyumba hiyo ni lazima ibomolewe na mawe yake, miti yake na lipu vipelekwe mahali najisi nje ya mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii hawana budi kuibomoa hiyo nyumba, nayo mawe yake na miti yake na takataka zote za hiyo nyumba sharti wazipeleke nje ya mji na kuzitupia mahali penye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hata mahali palipo na uchafu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyumba hiyo inapaswa kubomolewa na mawe yake, miti yake na lipu vipelekwe pahali pachafu inje ya muji.