Leviticus 14:48 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini ikiwa baada ya kuikagua nyumba hiyo, kuhani ataona kuwa upele haujaenea baada ya kupigwa lipu, basi, kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi kwani upele umekwisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa ukoma haujaenea tena baada ya nyumba kupakwa chokaa, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu ukoma umekwisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwamba kuhani akiingia ndani na kuangalia, na tazama, ikiwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba, baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atasema kwamba hiyo nyumba i safi, maana, pigo limepoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini ikiwa baada ya kuikagua nyumba hiyo, kuhani ataona kuwa upele haujaenea baada ya kupigwa lipu, basi, kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi kwani upele umekwisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha kuhani akiingia ndani kukagua na kuona kuwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi, maana pigo limepoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini ikiwa baada ya kuikagua nyumba hiyo, kuhani ataona kuwa upele haujaenea baada ya kupigwa lipu, basi, kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi kwani upele umekwisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtambikaji akiingia humo na kutazama, basi, akiona, ya kama huo ugonjwa mbaya haukuendelea humo nyumbani, walipokwisha kuipaka tena, mtambikaji hana budi kusema, ya kama hiyo nyumba imekwisha kutakata, kwa kuwa ugonjwa huo mbaya umepona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwamba kuhani akiingia ndani na kuangalia, na tazama, ikiwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba, baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atasema kwamba hiyo nyumba i safi, maana, pigo limepoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiwa kisha kuchunguza nyumba hiyo, kuhani akiona kwamba taka halikuenea kisha kupigwa lipu, basi, kuhani atatangaza kwamba nyumba hiyo ni safi maana taka limekwisha.