Leviticus 15:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote alichokalia mtu huyo, atakuwa najisi mpaka jioni. Mtu yeyote anayebeba kitu chochote kilichokuwa cha mtu huyo ni lazima ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na yeyote atakayegusa kitu chochote alichokuwa amekalia atakuwa najisi hadi jioni. Yeyote atakayeinua vitu hivyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu awaye yote atakayegusa kitu cho chote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hata jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote alichokalia mtu huyo, atakuwa najisi mpaka jioni. Mtu yeyote anayebeba kitu chochote kilichokuwa cha mtu huyo ni lazima ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na ye yote atakayegusa kitu cho chote alichokuwa amekalia atakuwa najisi mpaka jioni; ye yote atakayeinua vitu hivyo, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na yeyote atakayegusa kitu chochote alichokuwa amekalia atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayeinua vitu hivyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hadi jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote alichokalia mtu huyo, atakuwa najisi mpaka jioni. Mtu yeyote anayebeba kitu chochote kilichokuwa cha mtu huyo ni lazima ayafue mavazi yake, na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye kila atakayegusa cho chote kilichokuwa chini yake atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni, naye atakayevichukua vilivyo hivyo sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu awaye yote atakayegusa kitu cho chote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hata jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote atakayegusa kitu chochote mutu huyu alichoikalia atakuwa muchafu mpaka magaribi. Mutu yeyote anayebeba kitu chochote kilichokuwa cha mutu huyu anapaswa kufua nguo zake na kuoga. Atakuwa muchafu mpaka magaribi.