Leviticus 15:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwanamke yeyote anapokuwa mwezini, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Mtu yeyote atakayemgusa mwanamke huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwanamke yeyote anapokuwa mwezini, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Mtu yeyote atakayemgusa mwanamke huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na ye yote atakayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwanamke yeyote anapokuwa mwezini, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba. Mtu yeyote atakayemgusa mwanamke huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanamke akiingia miezini, atokwe na damu mwilini mwake, sharti atengwe siku saba, naye kila atakayemgusa atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke ye yote, kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichokuwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake muda wa siku saba; na mtu ye yote atakayemgusa atakuwa najisi hata jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke yeyote anapokuwa na ugonjwa wa mwezi, atakuwa muchafu kwa muda wa siku saba. Mutu yeyote atakayemugusa mwanamuke yule atakuwa muchafu mpaka magaribi.