Leviticus 15:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote atakayegusa cho chote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote anachokalia mwanamke huyo ni lazima ayafue mavazi yake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye kila atakayegusa cho chote, alichokikalia, sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu ye yote atakayekigusa cho chote ambacho huyo mwanamke amekiketia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote atakayegusa kitu chochote mwanamuke huyo anachoikalia anapaswa kufua nguo zake na kuoga kwa maji, naye atakuwa muchafu mupaka magaribi.