Leviticus 15:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama mwanamke anatokwa na damu kwa muda wa siku nyingi kuliko ilivyo kawaida au anatokwa damu wakati usio wa majira yake ya kutokwa damu, basi, ataendelea kuwa najisi muda wote damu inapomtoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu najisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama mwanamke anatokwa na damu kwa muda wa siku nyingi kuliko ilivyo kawaida au anatokwa damu wakati usio wa majira yake ya kutokwa damu, basi, ataendelea kuwa najisi muda wote damu inapomtoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama mwanamke anatokwa na damu kwa muda wa siku nyingi kuliko ilivyo kawaida au anatokwa damu wakati usio wa majira yake ya kutokwa damu, basi, ataendelea kuwa najisi muda wote damu inapomtoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanamke akitoka damu zake siku nyingi zisizo zake za kuwa miezini, au kama anatoka damu kuzipita hizo siku za kuwa miezini, basi siku zote za kutoka damu ni mwenye uchafu; kama alivyo akiwa miezini, ndivyo, mwenye uchafu alivyo siku hizo nazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye yu najisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mwanamuke anatokwa na damu kwa muda wa siku nyingi kuliko vile inavyokuwa kawaida au anatokwa damu wakati usiokuwa wa kawaida yake ya kutokwa damu, basi, ataendelea kuwa muchafu muda wote damu inapomutoka.