Leviticus 15:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kukauka damu yake mwanamke huyo atangoja hadi siku saba ili kuwa safi; na baada ya muda huo atakuwa safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa ametakasika kabisa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kukauka damu yake mwanamke huyo atangoja hadi siku saba ili kuwa safi; na baada ya muda huo atakuwa safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Wakati atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa safi kwa kawaida ya ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Wakati atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa safi kwa kawaida ya ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini huyo mwanamke akiwa ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kukauka damu yake mwanamke huyo atangoja hadi siku saba ili kuwa safi; na baada ya muda huo atakuwa safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akipata kutakata, kwa kuwa damu yake imekoma, sharti ahesabu siku saba, halafu atakuwa ametakata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya kukauka damu yake mwanamuke huyo atangoja bado siku saba kwa kuwa safi, na nyuma ya muda ule atakuwa safi.