Leviticus 15:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamtoa mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Hivyo kuhani atamfanyia huyo mwanamke ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumwondolea unajisi wake wa kutokwa damu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atatoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu kwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamtoa mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Hivyo kuhani atamfanyia huyo mwanamke ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumwondolea unajisi wake wa kutokwa damu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atatoa dhabihu, huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA kwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atatoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za bwana kwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamtoa mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Hivyo kuhani atamfanyia huyo mwanamke ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu na kumwondolea unajisi wake wa kutokwa damu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji na atengeneze mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya uchafu wake, damu zake ziliomtia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atatoa mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Hivyo kuhani atamufanyia huyo mwanamuke ibada ya upatanisho mbele ya Yawe na kumwondolea uchafu wake wa kutokwa damu.