Leviticus 15:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sheria hiyo yamhusu pia mwanamke anayetokwa damu na kuwa najisi. Sheria hiyo yamhusu mwanamume au mwanamke yeyote anayetokwa na chochote na pia yahusu mwanamume anayelala na mwanamke ambaye ni najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ya mwanamke ambaye yu katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, kama ni mtu mume, kama ni mtu mke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sheria hiyo yamhusu pia mwanamke anayetokwa damu na kuwa najisi. Sheria hiyo yamhusu mwanamume au mwanamke yeyote anayetokwa na chochote na pia yahusu mwanamume anayelala na mwanamke ambaye ni najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi kwa kawaida ya ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi kwa kawaida ya ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ya mwanamke ambaye yuko katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, awe ni mwanamume, au ni mwanamke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sheria hiyo yamhusu pia mwanamke anayetokwa damu na kuwa najisi. Sheria hiyo yamhusu mwanamume au mwanamke yeyote anayetokwa na chochote na pia yahusu mwanamume anayelala na mwanamke ambaye ni najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tena ya mwanamke akiingia miezini, nayo ya kila mwenye kisonono, kama ni mtu mume, au kama ni mtu mke, nayo ya mtu anayelala na mwanamke aliye mwenye uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ya mwanamke ambaye yu katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, kama ni mtu mume, kama ni mtu mke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sheria hiyo inaelekea vilevile mwanamuke anayetokwa damu na kuwa muchafu. Sheria hiyo inaelekea mwanaume au mwanamuke yeyote anayetokwa na chochote na vilevile inaelekea mwanaume anayelala na mwanamuke ambaye ni muchafu.