Leviticus 16:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ili asije akafa, atauleta ubani huo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuutia katika moto ili moshi wa ubani huo ukifunike kifuniko cha sanduku la agano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ataweka uvumba juu ya moto mbele za Mwenyezi Mungu, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili asife.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ili asije akafa, atauleta ubani huo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuutia katika moto ili moshi wa ubani huo ukifunike kifuniko cha sanduku la agano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ataweka uvumba juu ya moto mbele za BWANA, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili kwamba asife.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ataweka uvumba juu ya moto mbele za bwana, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili asife.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ili asije akafa, atauleta ubani huo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuutia katika moto ili moshi wa ubani huo ukifunike kifuniko cha sanduku la agano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Humo na ayatie hayo mavukizo juu ya moto mbele ya Bwana, moshi ya hayo mavukizo ukifunike Kiti cha Upozi kilichoko juu ya Sanduku la Ushahidi, asipate kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kusudi asikufe, ataleta ubani ule mbele ya Yawe na kuutia katika moto kusudi moshi wa ubani ule ufunike kifuniko cha Sanduku la Agano.