Leviticus 16:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha atatoka na kwenda kwenye madhabahu iliyo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuifanyia ibada ya upatanisho. Atachukua kiasi cha damu ya yule fahali na ya yule mbuzi na kuzipaka pembe za madhabahu pande zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha atatoka aje kwenye madhabahu yaliyo mbele za Mwenyezi Mungu na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi, na kuiweka kwenye pembe za madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha atatoka na kwenda kwenye madhabahu iliyo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuifanyia ibada ya upatanisho. Atachukua kiasi cha damu ya yule fahali na ya yule mbuzi na kuzipaka pembe za madhabahu pande zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha atatoka kuja kwenye madhabahu ile iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi na kuiweka kwenye pembe za madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha atatoka aje kwenye madhabahu yaliyo mbele za bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi, na kuiweka kwenye pembe za madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha atatoka na kwenda katika madhabahu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha atatoka na kwenda kwenye madhabahu iliyo mbele ya Mwenyezi-Mungu na kuifanyia ibada ya upatanisho. Atachukua kiasi cha damu ya yule fahali na ya yule mbuzi na kuzipaka pembe za madhabahu pande zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akitoka na afike penye meza ya kutambikia iliyoko mbele ya Bwana, aipatie upozi nayo akichukua damu kidogo ya yule dume la ng'ombe na ya dume la mbuzi, azipake pembe za meza ya kutambikia pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha atatoka na kwenda kwenye mazabahu inayokuwa mbele ya Yawe na kufanya ibada ya upatanisho. Atatwaa sehemu ya damu ya yule ngombe dume na ya yule mbuzi na kupakaa pembe za mazabahu pande zote.