Leviticus 16:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimwambia, “Mwambie ndugu yako Aroni asiingie mahali patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie mahali hapo kwani ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: “Mwambie ndugu yako Haruni asije wakati wowote anaotaka ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, nyuma ya pazia pale mbele ya kiti cha rehema kile kilicho juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimwambia, “Mwambie ndugu yako Aroni asiingie mahali patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie mahali hapo kwani ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamwambia Mose: “Mwambie ndugu yako Aroni asije wakati wo wote atakavyo yeye ndani ya Patakatifu pa Patakatifu nyuma ya pazia mbele ya kiti cha rehema kile kilichoko juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamwambia Musa: “Mwambie ndugu yako Haruni asije wakati wowote atakavyo yeye ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, nyuma ya pazia pale mbele ya kiti cha rehema kile kilichoko juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alimwambia, “Mwambie ndugu yako Aroni asiingie mahali patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie mahali hapo kwani ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hapo Bwana alimwambia Mose: mwambie kaka yako Haroni, asiingie wakati wo wote Patakatifu ndani ya kile chumba cha mbele ya lile pazia na kukitokea Kiti cha Upozi kilichoko juu ya hilo Sanduku, asipate kufa. Kwani mimi hutokea winguni juu ya hicho Kiti cha Upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamwambia: Umwambie ndugu yako Haruni asiingie katika Pahali Patakatifu nyuma ya pazia wakati usiokubaliwa. Asiingie pahali pale maana ndipo nitakapotokea katika wingu juu ya kiti cha rehema. Asipotii, atakufa.