Leviticus 16:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni ataweka mikono yake juu ya kichwa cha huyo beberu hai na kuuungama juu yake dhambi zote za watu wa Israeli, makosa yao yote na dhambi zao zote, ili kumwajibisha huyo. Kisha atamwacha huyo beberu aende jangwani akipelekwa huko na mtu yeyote anayejitoa kwa hiari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, ili kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni ataweka mikono yake juu ya kichwa cha huyo beberu hai na kuuungama juu yake dhambi zote za watu wa Israeli, makosa yao yote na dhambi zao zote, ili kumwajibisha huyo. Kisha atamwacha huyo beberu aende jangwani akipelekwa huko na mtu yeyote anayejitoa kwa hiari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, kisha kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, ili kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, na dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atapelekwa jangwani na mtu aliyetayarishwa kwa ajili ya kazi hiyo
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni ataweka mikono yake juu ya kichwa cha huyo beberu hai na kuuungama juu yake dhambi zote za watu wa Israeli, makosa yao yote na dhambi zao zote, ili kumwajibisha huyo. Kisha atamwacha huyo beberu aende jangwani akipelekwa huko na mtu yeyote anayejitoa kwa hiari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Haroni na aibandike mikono yake yote miwili kichwani pake huyu dume la mbuzi aliye mzima bado, aungame juu yake manza zote za wana wa Isiraeli na mapotovu yao yote na makosa yao yote, ayatwike kichwani pake huyu dume la mbuzi, kisha na ampe mtu aliyewekwa kuwa tayari, ampeleke nyikani, ajiendee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni ataweka mikono yake juu ya kichwa cha huyo beberu muzima na kuungama juu yake zambi zote za watu wa Israeli, makosa yao yote na zambi zao zote; naye ataziweka zote juu ya kichwa cha yule mbuzi. Kisha atamwacha huyo beberu aende katika jangwa akipelekwa kule na mutu yeyote anayekuwa tayari.