Leviticus 16:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atamwacha huyo beberu aende jangwani, mahali pasipokuwa na watu, akiwa ameyachukua maovu yao yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote hadi mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atamwacha huyo beberu aende jangwani, mahali pasipokuwa na watu, akiwa ameyachukua maovu yao yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyokaliwa na watu; kisha atamwacha aende jangwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atamwacha huyo beberu aende jangwani, mahali pasipokuwa na watu, akiwa ameyachukua maovu yao yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye huyu dume la mbuzi na azichukue manza zao zote alizotwikwa, azipeleke katika nchi isiyokaa watu; huko nyikani ndiko amwachilie, ajiendee.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atamwacha huyo beberu aende katika jangwa, pahali pasipokuwa watu, akiwa amebeba maovu yao yote.