Leviticus 16:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule fahali na mbuzi waliotolewa sadaka ya kuondoa dhambi ambao damu yao ilipelekwa mahali patakatifu sana ili kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa nje ya kambi na kuteketezwa. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule fahali na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi. Ngozi zao, nyama, na matumbo vitateketezwa kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule fahali na mbuzi waliotolewa sadaka ya kuondoa dhambi ambao damu yao ilipelekwa mahali patakatifu sana ili kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa nje ya kambi na kuteketezwa. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule fahali na mbuzi aliyetolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi; ngozi zao, nyama, na matumbo yake pamoja na mavi vitateketezwa kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule fahali na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi. Ngozi zao, nyama, na matumbo pamoja na mavi vitateketezwa kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya kambi; nao watateketeza ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule fahali na mbuzi waliotolewa sadaka ya kuondoa dhambi ambao damu yao ilipelekwa mahali patakatifu sana ili kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa nje ya kambi na kuteketezwa. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye dume la ng'ombe aliye ng'ombe ya tambiko ya weuo naye dume la mbuzi aliye ng'ombe ya tambiko ya weuo, ambao damu zao zilipelekwa Patakatifi za kupozea mumo humo, na awapeleke nje ya makambi, wateketeze huko kwa moto ngozi zao na nyama zao na mavi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule ngombe dume na mbuzi waliotolewa sadaka kwa ajili ya zambi ambao damu yao ilipelekwa katika Pahali Patakatifu kwa kufanya ibada ya upatanisho, watapelekwa inje ya kambi na kuteketezwa kwa moto. Ngozi zao, nyama na mavi yao, vyote vitateketezwa kwa moto.