Leviticus 16:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hili ni sharti ambalo mnapaswa kulifuata milele: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, nyinyi wenyewe na hata wageni wanaoishi miongoni mwenu, ni lazima mfunge siku hiyo na kuacha kufanya kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge, wala msifanye kazi yoyote, iwe mzawa au mgeni anayeishi miongoni mwenu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hili ni sharti ambalo mnapaswa kulifuata milele: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, nyinyi wenyewe na hata wageni wanaoishi miongoni mwenu, ni lazima mfunge siku hiyo na kuacha kufanya kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge wala msifanye kazi yo yote akiwa mzaliwa au mgeni anayeishi miongoni mwenu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge, wala msifanye kazi yoyote, iwe mzawa au mgeni anayeishi miongoni mwenu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajinyima, msifanye kazi ya namna yoyote, mzaliwa na mgeni akaaye kati yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hili ni sharti ambalo mnapaswa kulifuata milele: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, nyinyi wenyewe na hata wageni wanaoishi miongoni mwenu, ni lazima mfunge siku hiyo na kuacha kufanya kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya na yawe kwenu maongozi ya kale na kale: katika mwezi wa saba siku ya kumi ya mwezi huu sharti mjitese wenyewe, msifanye kazi yo yote, wala wenyeji wala wageni walioko kwenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hili ni sharti la kufuata siku zote: Siku ya kumi ya mwezi wa saba, ninyi wenyewe na hata wageni wanaoishi kati yenu, munapaswa kufunga kula siku hiyo na kuacha kufanya kazi.