Leviticus 16:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo ni siku ya mapumziko kamili nanyi mtafunga. Kanuni hiyo ni ya kudumu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo ni siku ya mapumziko kamili nanyi mtafunga. Kanuni hiyo ni ya kudumu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni Sabato ya mapumziko, ni lazima mfunge; ni agizo la kudumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajinyima; ni amri ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo ni siku ya mapumziko kamili nanyi mtafunga. Kanuni hiyo ni ya kudumu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo ya mapumziko sharti iwe kwenu ya mapumziko kabisa; ndipo, mtakapojitesa kwa kufunga. Haya ndiyo maongozi ya kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo ni siku ya mapumziko kamili nanyi mutafunga. Hili ni sharti la kufuata siku zote.