Leviticus 17:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama mtu yeyote wa jumuiya ya Israeli au mgeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamwandama mtu huyo aliyekula damu na kumtenga mbali na watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakula damu yoyote, nitakuwa kinyume chake, na nitamkatilia mbali na watu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama mtu yeyote wa jumuiya ya Israeli au mgeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamwandama mtu huyo aliyekula damu na kumtenga mbali na watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye hunywa damu yo yote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakunywa damu yoyote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama mtu yeyote wa jumuiya ya Israeli au mgeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamwandama mtu huyo aliyekula damu na kumtenga mbali na watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli, hata mgeni atakayekaa kwao, atakayekula damu yo yote, mtu huyu atakayekula damu nitamkazia macho yangu, nimng'oe katikati yao walio ukoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu yeyote wa jamii ya Israeli au mugeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamukasirikia mutu yule aliyekula damu na kumutenga mbali na watu wake.