Leviticus 17:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, uhai wa kila kiumbe umo katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, kamwe wasile damu ya kiumbe chochote kwani uhai wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msile damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, uhai wa kila kiumbe umo katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, kamwe wasile damu ya kiumbe chochote kwani uhai wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe cho chote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; ye yote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; yeyote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe uko katika damu yake; ndio nikawaagiza wana wa Israeli, Msiile damu ya mnyama wa aina yoyote; kwa kuwa uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayeila atatengwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, uhai wa kila kiumbe umo katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, kamwe wasile damu ya kiumbe chochote kwani uhai wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, maana humu ndimo, roho yake ilimo; kwa hiyo nimewaambia wana wa Isiraeli: Msile damu zao wo wote walio wenye miili! Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, naye kila atakayeila sharti ang'olewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, uzima wa kila kiumbe uko katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, wasikule damu ya kiumbe chochote maana uzima wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.