Leviticus 17:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni; kisha atakuwa ametakaswa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mtu ye yote, awe mzaliwa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu cho chote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzaliwa au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kila atakayekula kibudu au nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine, kama ni mwenyeji au kama ni mgeni, sharti azifue nguo zake na koga majini, naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni, kisha atakuwa ametakata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote akuwe ni mwenyeji au mugeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na nyama wa pori anapaswa kufua nguo zake na kuoga. Atakuwa muchafu mpaka magaribi. Nyuma ya hapo atakuwa safi.