Leviticus 17:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
badala ya kumleta mnyama huyo kwenye mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu mbele ya maskani yake takatifu, mtu huyo atakuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu na atatengwa na watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu mbele ya Maskani ya Mwenyezi Mungu, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu, na ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, ili amtoe kuwa matoleo kwa Bwana mbele ya hema ya Bwana; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
badala ya kumleta mnyama huyo kwenye mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu mbele ya maskani yake takatifu, mtu huyo atakuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu na atatengwa na watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa BWANA mbele ya Maskani ya BWANA, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa bwana mbele ya Maskani ya bwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, kama matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na atatupiliwa mbali na watu wake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
badala ya kumleta mnyama huyo kwenye mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu mbele ya maskani yake takatifu, mtu huyo atakuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu na atatengwa na watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
asimpeleke pa kuliingilia Hema la Mkutano, amtolee Bwana toleo la tambiko mbele ya Kao lake Bwana, mtu huyu na awaziwe kuwa mwenye manza za damu: kwa kuwa alimwaga damu, sharti ang'olewe mtu huyu katikati yao walio ukoo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, ili amtoe kuwa matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
bila kumuleta nyama huyo kwenye mulango wa hema la mukutano kwa kumutolea Yawe mbele ya makao yake, mutu yule atakuwa na kosa ya kumwanga damu. Amemwanga damu na atatengwa na watu wake.