Leviticus 17:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kusudi la sheria hii ni kwamba Waisraeli wanapaswa kuleta wanyama ambao wangewachinjia mashambani ili wawalete kwa Mwenyezi-Mungu kwa kuhani kwenye mlango wa hema la mkutano, naye atawachinja na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ni ili Waisraeli wamletee Mwenyezi Mungu dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Mwenyezi Mungu, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kuwa sadaka za amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili kusudi wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, naam, wazilete kwa Bwana, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kusudi la sheria hii ni kwamba Waisraeli wanapaswa kuleta wanyama ambao wangewachinjia mashambani ili wawalete kwa Mwenyezi-Mungu kwa kuhani kwenye mlango wa hema la mkutano, naye atawachinja na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ni ili kwamba Waisraeli wamletee BWANA dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa BWANA, katika ingilio la Hema la Kukutania na kutoa dhabihu kama sadaka za amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ni ili Waisraeli wamletee bwana dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa bwana, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kama sadaka za amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, wazilete kwa BWANA, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kusudi la sheria hii ni kwamba Waisraeli wanapaswa kuleta wanyama ambao wangewachinjia mashambani ili wawalete kwa Mwenyezi-Mungu kwa kuhani kwenye mlango wa hema la mkutano, naye atawachinja na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka za amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kwamba: ng'ombe zao za tambiko, wanazozichinja maporini, wana wa Isiraeli sharti wampelekee Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano na kumpa mtambikaji, ndipo wazichinje kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani za Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili kusudi wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, naam, wazilete kwa BWANA, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Agizo hili linalazimisha Waisraeli kuletea Yawe nyama ambao wanawachinja katika mashamba. Wataleta nyama wale kwa kuhani kwenye mulango wa hema la mukutano, naye atawachinja na kumutolea Yawe sadaka za amani.