Leviticus 17:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kuhani atainyunyizia damu madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyoko mlangoni mwa hema la mkutano na kuyateketeza yale mafuta yawe harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Mwenyezi Mungu katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kuhani atainyunyizia damu madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyoko mlangoni mwa hema la mkutano na kuyateketeza yale mafuta yawe harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya BWANA katika ingilio la Hema la Kukutania na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya bwana katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kuhani atainyunyizia damu madhabahu ya Mwenyezi-Mungu iliyoko mlangoni mwa hema la mkutano na kuyateketeza yale mafuta yawe harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo damu mtambikaji na azinyunyize juu ya meza ya kumtambikia Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, nayo mafuta na ayateketeze kuwa moshi wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kuhani atanyunyizia damu kwenye mazabahu ya Yawe inayokuwa kwenye mulango wa hema la mukutano na kuteketeza yale mafuta yakuwe harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.