Leviticus 18:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Usimtoe kafara mtoto wako yeyote kwa Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Usimtoe mtoto wako ye yote awe kafara kwa mungu Moleki, kamwe usilinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usimtoe kafara mzaliwa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utalikufuru jina langu mimi Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo miongoni mwao walio wa uzao wako usitoe hata mmoja wa kumpa Moloki, wamwingize motoni, usipate kulichafua Jina la Mungu wako. Mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usimutoe mutoto wako yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki maana kufanya hivyo utazarau jina langu mimi Mungu wako. Mimi ni Yawe.