Leviticus 18:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yo yote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi BWANA Mungu wako.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wako.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo yaangalieni, niliyowaambia, yanayowapasa kuyaangalia, msiyafuate na kuyafanya yale maongozi yatapishayo, yaliyofanywa mbele yenu, msijipatie uchafu kwa kuyafanya. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo mushike kwa ukamilifu yote ninayowaagiza. Musifuate tabia zozote ya kuchukiza zilizofanywa na wale walioishi katika inchi mbele yenu, kusudi musijichafue kwa njia yake. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.