Leviticus 18:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, ili mtu apate kuyaokoa maisha, mnapaswa kuyashika masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, ili mtu apate kuyaokoa maisha, mnapaswa kuyashika masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mzishike amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu; yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, ili mtu apate kuyaokoa maisha, mnapaswa kuyashika masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo yaangalieni maongozi yangu! Naye mtu ye yote atakayeyafanya maamuzi yangu atapata uzima kwa njia hiyo, maana mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapaswa kushika masharti yangu na maagizo yangu: yule anayeyashika ataishi. Mimi ni Yawe.