Leviticus 19:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Usiende huko na huko ukieneza uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu cho chote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidishe kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
usitembee kwa wenzako wa ukoo, upate mtu wa kumchongea. Usitoe ushahidi wa uwongo wa kumwua mwenzako. Mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usipitepite hata kidogo ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usitie maisha ya mwenzako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ni Yawe.