Leviticus 19:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mjakazi aliyeposwa na mwanaume mwingine, ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtu ye yote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mume, wala hakukombolewa kwa lo lote, wala hakupewa uhuru; wataadhibiwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama mwanaume atakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mtu yeyote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mwanamume mwingine, wala hakukombolewa kwa lolote, wala hakupewa uhuru wake; watachunguzwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akilala kwa mwanamke kijakazi na kumpa mimba, naye alikuwa ameposwa na mtu mwingine, basi, akiwa hakukombolewa wala hakufunguliwa kujiendea, na wapatilizwe, lakini wasiuawe, kwa kuwa yule mwanamke hakufunguliwa kujiendea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtu ye yote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mume, wala hakukombolewa kwa lo lote, wala hakupewa uhuru; wataadhibiwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanaume akilala na mwanamuke mujakazi ambaye amechumbiwa na mwanaume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamuke huyo hakukuwa bado huru.